News
Seneta Cherargei, Anataka Waziri Murkomen Kujiuzulu
Baadhi ya viongozi wa kisiasa wamemtaka Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen kujiuzulu kwa madai kwamba ameshindwa kuimarisha usalama katika maeneo mbalimbali ya taifa.
Wakiongozwa na Seneta wa Nandi Samson Cherargei, Viongozi hao wamesema Waziri Murkomen umeonyesha wazi kutowajibika katika majukumu yake pamoja na kushindwa kupanga kikamilifu usalama wa taifa.
Cherargei amemtaka rais William Ruto kumhamisha Waziri Murkomen katika Wizara hiyo na kumpa wadhfa wa ubalozi katika mataifa ya Pakistan, Gaza ama nchini Tanzania ili kushughulikia masuala ya kidiplomasia.
Cherargei anasema masuala ya usalama huwezi kufananisha na masuala ya barabara kwani usalama wa wananchi ni muhimu zaidi na kutowajibika kwa Waziri Murkomen kumechangia wakaazi wa maeneo ya Kerio Valley kupoteza maisha yao.