International News

Rais Samia Suluhu wa CCM, aidhinishwa kugombea Urais Tanzania, Wapinzani Wakizuiliwa

Published

on

Tume ya uchaguzi nchini Tanzania, INEC imemuidhinisha rasmi Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, na mgombea mwenza Emmanuel Nchimbi kuwa wagombea wa Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM nchini humo.

Hatua hii imewekwa wazi kwamba Rais Samia huenda hatakuwa na upinzani mkubwa wakati wa uchaguzi mkuu utakapoandaliwa nchini humo baadaye Oktoba 29 mwaka huu baada ya tume hiyo kuwazuia wagombea wa vyama vikuu vya upinzani kushiriki uchaguzi huo.

Rais Samia Suluhu na mgembea mwenza Emmanuel Nchimba, sasa watakabiliana na wagombea wa vyama vidogo vidogo baada ya chama kikubwa cha upinzani CHADEMA, kinachooongozwa na Tundu Lisu, kuondolewa kwenye kinyang’anyiro hicho mnamo April 2025 kwa madai ya kukiuka na kukataa kutia saini makubaliano ya utaratibu na sheria za Uchaguzi.

Chama kingine cha upinzani kuondolewa hivi punde ni kile cha Alliance for Change and Transparency ACT- Wazalemdo kinachoongozwa na Luhaga Mpina.

Luhaga amekatazwa kushiriki uchaguzi huo na tume hiyo ya Uchaguzi, INEC.

Kinara wa cha chama cha ACT – Wazalendo, Luhaga Mpina.

Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA Tundu Lissu, amekuwa kizuizini kwa zaidi ya miezi mine sasa baada ya kushtakiwa kwa kosa la Uhaini mwezi April mwaka huu.

Hata hivyo Tundu amekanusha madai hayo akisema kuwa ni njama ya CCM kuhujumu Upinzani katika ushirikishwaji wa uchaguzi mwaka huu.

Kukamatwa kwa Lissu na pamoja na kuongezeka kwa visa vya utekaji nyara wa wanaharakati wa haki za bimadamu nchini Tanzani, kumeipa doa serikali ya Samia Suluhu Hassan katika kujitolea kwake kudumisha haki na usawa, licha ya rais huyo kusisitizia Ulimwengu kwamba amejitolea kudumisha haki za binadamu.

Miongoni mwa visa vya utekaji nyara hivi majuzi ni Wakenya waliokuwa wamesafuiri nchini humo kufuatilia kesi ya Tundu Lisu, wakiongozwa na Martha Karua, Jaji mkuu mstaafu Willy Muntunga na mwanaharakati Boniface Mwangi.

Rais Suluhu aliingia mamlakani kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Nchi hiyo John Pombe Magufuli kufariki 2021

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version