Business
Paul Katana: Serikali fufua viwanda Kilifi
Wito umetolewa kwa serikali kuu kufufua viwanda vilivyofungwa katika kaunti ya kilifi ili kubuni nafasi zaidi za ajira.
Mbunge wa Kaloleni Paul Katana, alisema kuna viwanda vingi kaunti ya kilifi ambavyo kwa sasa vimefungwa jambo ambalo linafanya uchumi wa eneo hili kudorora.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa Katana alisema kuwa wananchi wengi wanapitia changamoto kutokana na ukosefu wa ajira, hivyo kufufuliwa kwa viwanda hivyo kutainua uchumi na maisha kwa jumla.
Katana aliongeza kuwa tangu taifa lipate uhuru, wakaazi wa eneo hilo bado wanaishi maisha duni kutokana na ukosefu wa ajira kwa vijana na miundombinu duni.
Wakati huo huo kiongozi huyo aliwataka wanachi kutokubali kuhadaiwa na viongozi ambao hawawezi kuwaletea maendeleo, akiwataka kujiunga na serikali jumuishi ili kuweza kunufaika na kutatuliwa shida zao.
Taarifa ya Pauline Mwango