News

Owen, Akubali kuondoa mswada wa kuharimisha Mugoka bungeni

Published

on

Naibu Rais Prof Kithure Kindiki amesema kuna matumaini ya kuondolewa kwa mswada unaolenga kuharamisha mzao la Mugoka ambao ulikuwa umewasilishwa bungeni.

Kindiki alisema hatua hiyo ni kufuatia mkutano ulioandaliwa kati ya ofisi yake, viongozi kutoka Embu wakiongozwa na Gavana wa Embu Cecily Mbarire pamoja na Mbunge wa Kilifi Kazkazini Owen Baya ambaye alikuwa amewasilisha mswada huo bungeni.

Katika Mkutano huo ambao ulifanyika katika makao makuu ya Naibu rais katika eneo la Karen, Kindiki aliweka wazi kwamba zao hilo ambalo linakuzwa kwa wingi katika eneo hilo ni kati ya mazao ya kibiashara na mswada uliyokuwa umewasilisha bungeni ungeondoa zao hilo kwenye orodha ya mazao ya kibiashara nchini.

“Tumeafikiana mambo kadhaa kuhusu mswada huo kutokana na shinikizo nilizopokea kutoka kwa wakulima wa zao la Mugoka na  kuafikiana kwamba Mheshimiwa Baya ataondoa mswada huo bungeni”, alisema Naibu Rais.

Naibu rais Prof Kithure Kindiki na Mbunge wa Kilifi Kazkazini Owen Baya wafanya mazungumzo.

Mswada huo uliwasilishwa bungeni na Mbunge wa Kilifi Kazkazini Owen Baya akilenga kuondoa zao la Mugoka katika orodha ya mazao ya kibiashara kutokana na zao hilo kuorodheshwa kuwa kati ya mazao yenye athari kubwa kwa maisha ya binadamu na umekuwa ukiathiri vijana wengi hasa eneo la Pwani.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version