Sports
Nyota wa Liverpool Diego Jota Aaga Dunia.
Mshambulizi wa Liverpool Diogo Jota amefariki dunia kufuatia ajali ya gari nchini Uhispania akiwa na umri wa miaka 28, vyombo vya habari vya Ureno vimeripoti.
Inasemekana Jota alikuwa akisafiri kwa gari pamoja na kaka yake Andre, ambaye pia ni mwanasoka mwenye umri wa miaka 26.
Tukio hilo lilitokea katika jimbo la Zamora wiki mbili tu baada ya Jota kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Rute Cardoso huko Porto.