Sports
Mabondia Kutoka Vilabu Mbalimbali Nchini, Kuzindua Uhasama Mjini Mombasa
Zaidi ya mabondia 180 wa kiwango cha juu kutoka vilabu 26 kote nchini wanatarajiwa kushiriki mashindano ya ndondi ya mzunguko wa pili Kenya yanayotarajiwa kuanza hii leo hadi 19 mwaka huu yatakayoandaliwa katika taasisi ya Alliance Francaise jijini Mombasa.
Miongoni mwa mabondia watakaoshiri mashindano hayo ni Bonface Mogunde wa huduma ya polisi nchini ambaye hajapoteza pambano katika uzani wake, mshindi wa dhahabu kwenye Michezo ya Afrika Edwin Okongo wa KDF mabondia wa Mombasa, Kombo Mwinyifaki na Shaffi Bakari, pia watapanda ulingoni.
Mashindano hayo yameandaliwa na chama cha Ndondi cha Kaunti ya Mombasa kwa ushirikiano na taasisi ya Alliance Française kama sehemu ya mradi wa ushirikiano wa michezo kati ya Kenya na Ufaransa uitwao Ndondi Mashinani, kwa usaidizi wa Ubalozi wa Ufaransa.
Michuano hiyo inalenga kukuza vipaji, hasa kwa wanawake na vijana, pamoja na kuandaa wawakilishi wa Mombasa kwa mashindano ya Olimpiki yajayo.