International News
Raila Azungumza Baada ya Kuanguka Uchaguzi wa AUC
Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Tume ya umoja wa Afrika, AUC, kutoka Kenya, Raila Odinga, amevunja kimya chake na kuzungumzia uchanguzi wa nafasi hiyo uliyofanyika siku ya Jumamosi.
Akihutubia wajumbe wakenya akiwa jijini Addis Ababa nchini Ethiopia, Odinga amesema wakenya wanafaa kusitisha uvumi kwamba alishindwa kutokana na uzee, ama kukosa kufanya kampeni bora.
Odinga amesema kuna maswala muhimu ambayo yanafaa kuangaziwa ili changuzi zijazo iwe rahisi kwa Kenya kunyakua kiti hicho na wala sio kwa wakenya kuendeleza propaganda zisizo na manufaa yoyote.
Odinga hata hivyo amempogeza rais William Ruto kwa kuhakikisha kampeni zake zinafanyika vyema sawa na kumpangia vikao na marais wa mataifa ya Afrika ili kutafuta uugwaji mkono, japo hakufaulu.