Sports

Nataka Stars Kwenye Fainali Ya Chan Asema Mvurya

Published

on

Waziri wa Michezo Salim Mvurya amesema kwamba lengo lake ni kuona timu ya Soka Harambee Stars katika fainali ya kombe la CHAN linalongoa nanga mwezi ujao hapa nchini.

Akizungumza na wanahabari Mvurya amesema kwamba miondo misingi iko tayari na wanaipa timu ya soka kila kitu kufanya vyema katika mashindano hayo yanayoandaliwa kwa mara ya kwanza katika nchi za Afrika Mashariki Kenya,Uganda na Tanzania.

“Kwa sasa naweza nikathibitishia Wakenya tuko vizuri kwa kombe la CHAN,kuna wakati timu zetu zimkeua zikitatizika mpaka kucheza mechi za kufuzu nje ya nchi kwani hatukua na uwanja wa kutumia ila sasa ni furaha kuwa na viwanja vya viwango kama Kasarani na Nyayo.”

Waziri huyo ameongezea kwamba kwa sasa Stars ina kocha mwenye tajriba na serikali kupitia kwa Wizara yake itaipa sapoti kocha huyo kuleta matokeo chanya.

Kwa mujibu wa Mvurya itakua vyema zaidi Stars wakifika Fainali ambayo inachezwa ugani Kasarani Agosti 30.

“Lengo letu ni kuona Stars kwenye Fainali maanake itakua bora zaidi fainali inaypigwa Kasarani,mashabiki wajitokezee tusapoti vijana wa nyumbani.”

Stars wanafungua kampeini yao dhidi ya DR.Congo Agosti 3 ugani Kasarani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version