News
Mungatana, akosoa harakati za kisiasa za Gachagua
Viongozi wa kaunti ya Tanariver wamepuuza harakati za kisiasa za Kinara wa chama cha Democracy for the Citizen’s Party- DCP, Rigathi Gachagua wakimtaja kama kiongozi anayeendeleza ukabila humu nchini.
Wakiongozwa na Seneta wa kaunti hiyo Danson Buya Mungatana, viongozi hao wamesema kuwa Gachagua hana sera isipokuwa kumtusi na kumkejeli rais William Ruto.
Aidha wamesema kuwa kamwe hawataacha kusimama na serikali inayounganisha wakenya wote hususan baada ya Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga kuungana na rais William Ruto kuimarisha utendakazi wa serikali.
Wakizungumza katika kaunti hiyo, viongozi hao wamesisitiza haja ya wakaazi wa kaunti ya Tanariver kuunga mkono serikali tawala ili kunufaika kimaendeleo hasa mashinani.
Taarifa ya Hamis Kombe