Entertainment

#COCODRIVE: Crack Sound Siyo Mashine, Ni Vichwa – J Crack Asema Baada ya Kuibiwa Vyombo Studioni Kwake

Published

on

Mmiliki wa Crack Sound Records, J Crack, amepata pigo kubwa baada ya studio yake kuvamiwa na wezi walioiba vyombo vyake vya studio.

Akizungumza na kipindi cha Coco Drive cha COCO FM, msanii huyo alieleza kwa masikitiko jinsi wezi walivyoiba kila kitu, kuanzia vifaa vya muziki hadi mali ndogo ndogo za studio.

“Wameiba hadi kufuli ya mlango, computer ya kazi niliyotoka nayo Ulaya, laptop, TV mbili za reception na studio, electric guitar, piano… CCTV nimenunua sasa baada ya kuibiwa,” alisema J Crack kwa majonzi.

Kisa hiki kimewavunja moyo wasanii waliokuwa wakifanya kazi chini ya lebo hiyo, ikiwemo Susumila, ambaye pia alikuwa na mradi wake binafsi studioni humo.

J Crack pia alidokeza kwamba alikuwa akipanga kuachia EP mpya, lakini sasa mipango hiyo imelazimika kusimama kwa muda kufuatia hifadhi ya EP yake kuibwa pamoja na vyombo vyake.

Licha ya kupoteza mali nyingi, J Crack anasema hana mpango wa kukata tamaa.

“Mwizi hajanikata miguu. Crack Sound siyo mashine, ni vichwa. Wangenikata kichwa hapo sasa wangekuwa wamenimaliza. Tunaendelea mbele,” alisisitiza.

J Crack pia alisema kwamba Susumila ambaye alipata taarifa hizo aliahidi kumsaidia kuwapata walihusika kutekeleza wizi huo akisema kwamba atayashughulikia kinyumbani.

“Susumila aliniambie tumuachie yeye, halafu sisi tudeal na polisi,” alisema kwa msisitizo.

Mashabiki wa muziki wameeleza masikitiko yao mtandaoni, wakimtakia J Crack na timu yake nguvu mpya na kurejea kwa kasi kwenye game.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version