Entertainment

Msanii Ndiye Amezaa Mwanaharakati, Chibo Dee Avunja Ukimya

Published

on

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Chibo Dee amevunja ukimya na kueleza kwa kina sababu zilizompelekea kuonekana kuisifu serikali, akijibu kwa hisia ukosoaji kutoka kwa blogger aliyemhoji kama ni “msanii, mwanaharakati ama chawa wa wanasiasa?”

Katika ujumbe aliouandika kupitia Facebook, Chibo Dee alifunguka kuhusu safari yake ya sanaa iliyojaa mapambano, akieleza kuwa kabla ya watu kumwelewa vibaya leo, alikuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za wananchi kupitia kazi yake ya muziki.

“Msanii ndiye amezaa mwanaharakati. Back in 2019 August, nilipokuwa naendeleza harakati za kutetea mwananchi na kukosoa serikali nilikuwa peke yangu. Nilitumia sanaa kuonyesha haki na bora ila nilijikuta matatani kwa kupelekwa polisi. Ila nilitolewa na wanasiasa. Wiki mbili ukiwa locker 😭😭😭.”

Chibo Dee anasema kuwa aliwahi kupitia wakati mgumu, ambapo harakati zake zilimpeleka rumande kwa zaidi ya wiki mbili. Kulingana naye, ni msaada wa kisiasa uliomtoa kutoka hali hiyo – jambo ambalo sasa linafanya wengine kumtazama tofauti.

Ujumbe huo ni jibu la moja kwa moja kwa blogger ambaye awali aliandika: “Chawa, Mwanaharakati au Msanii? – Chibo Dee,”  akiambatanisha picha ya msanii huyo, hatua iliyozua mjadala mkali mitandaoni.

Lakini kwa waliofuatilia safari ya Chibo Dee tangu mwaka 2019, ujumbe wake unadhihirisha kuwa sanaa kwake haikuwa tu burudani – bali chombo cha kupigania haki, na njia ya kuwasemea wasio na sauti.

Mara baada ya taarifa hiyo kusambaa, wafuasi na watumiaji wa mitandao walijitokeza na kutoa maoni yao. Baadhi walimtetea Chibo Dee, huku wengine wakionekana kumtupia lawama au dhihaka.

Maico Charly KE:
“Inawauma nini kwani si ni maisha yake… watu wengine bhana… mtandaoni kutwa kufuatilia watu tu!”

Kensam Kijazo:
“Njaaa inamsumbua, muacheni apate mkate wake.”

Nicko Wangu:
“Chibo Dee, piga kazi mwanangu. Chawa sio wewe – admin ndiye kibaraka wa Asha Jumwa, uwe mwelewa mdogo wangu!”

Chibo Dee ni miongoni mwa waimbaji waliotumbuiza waombolezaji kwenye mazishi ya babake gavana wa kaunti ya Kilifi, Gideon Maitha Mung’aro, Gideon Baya Mung’aro aliyeaga dunia mwezi Juni 15, 2025.

Mazishi hayo yalifanyika wadi ya Dabaso, Kilifi Kaskazini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version