News
Mpango wa matumizi ya kawi safi Kilifi kukabili mabadiliko ya hali ya anga
Kongamano la siku tatu kuhusu wiki ya upishi kutumia kawi safi limezinduliwa rasmi mjini Kilifi katika kaunti ya Kilifi huku serikali kuu ikimesema inaendelea kujumuisha kila eneo katika miradi mbali mbali ya maendeleo.
Waziri wa Kawi nchini Opiyo Wandayi alisema serikali kuu inashirikisha serikali za kaunti kwenye mipango ya kawi safi ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Akizungumza katika kongamano hilo, waziri Wandayi alisema Kenya inaendelea kutekeleza matumizi ya kawi safi ili kuepuka athari za kiafya kwa watumizi pamoja uharibifu wa Mazingira.
Waziri Wandayi alisistiza kuwa kwa sasa serikali inauia kuafikia utekelezaji wa sheria na mipango ya kawi safi kwa kushirikiana na wadau tofauti kwa manufaa ya jamii.
Vile vile alidokeza kuwa serikali imeitegengea kaunti ya Kilifi zaidi ya shilingi bilioni 2 zitakazotumika kuunganisha nyumba elfu 21 za ziada na nguvu za umeme.
Kwa upande wake mkewe rais Bi Rachel Ruto alisema mpango huo wa upishi safi utakomoa familia nyingi mashinani kiuchumi, kuimarisha mazingira ya elimu kwa wanafunzi majumbani vile vile kuondoa kero la wanawake katika matumizi ya mbinu za kale za upishi.
Naye gavana wa kaunti ya Kilifi Gedion Mung’aro alisema mabadiliko ya tabia nchi yamekuwa na athari kubwa kwa wakaazi hasa maeno ya Ganze na Magarini, akisistiza kuwa kawi safi pekee itaokoa maisha ya wakaazi wengi.
Mama wa taifa Bi Rachel Ruto pamoja na Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro na Waziri wa Kawi nchini Opiyo Wandayi
Ubalozi wa Uingereza na Ujerumani hapa nchini ulishinikiza serikali kukumbatia kikamilifi matumizi ya kawi safi kwa kuafikia maendeleo endelevu sawa na kubuni nafasi zaidi za ajira, kwa kushirikiana na serikali za kaunti.
Kongamano hilo linatarajiwa kukamilika alhamisi Agost 28, 2025, kauli mbiu ikiwa ni kutekeleza mikakati na mipango ya upishi safi, mabadiliko, ushirikishwaji na uwezeshaji.
Taarifa ya Joseph Jira