Entertainment

Mbilia Bel Anusurika Kwenye Ajali ya Barabarani – Kinshasa

Published

on

Mwanamuziki mashuhuri wa Congo (DRC) Mbila Bel, anaendelea kupata matibabu katika Hospitali Moja Mjini Kinshasa, baada ya Gari alimokuwa akisafiria kuhusika kwenye ajali ya barabarani Septemba 9.

Kwa mujibu wa taarifa za vyanzo vya habari mjini Kinshasa, Mama Mbila Bel alikuwa safarini kuelekea uwanja wa Ndege wa N’djili, ili kuabiri Ndege akiwa na meneja wake wa muziki Jules Nsana ambaye pia alijeruhika

Mbila Bel ambaye jina lake halisi ni Marie Claire Mboyo, alitarajiwa kusafiri kuelekea nchini Ubelgiji kuwatumbuiza mashabiki wake katika ukumbi wa Madeleine Jijini Brussels, wakati ajali hiyo ilipotokea, baada ya dereva wake kushindwa kulithibiti gari lao.

Hali yake ya kiafya inatajwa kuwa mbaya na anahitaji Kwa dharura huduma za upasuaji na kina mipango ya kumhamishia Hospitali nyingine kwa matibabu zaidi.

Mbila Bel alizaliwa January 10 1959 na kupindukia kuwa maarufu kimuziki kunako miaka ya 70 alipojiunga na bendi ya Afrisa international ikiongozwa na Pascal Tabu Ley Rochereau.

Miongoni mwa nyimbo zake zilizotoa fora ni pamoja na Eswi Yo Wapi, Tempelo, Mpeve Ua Longo, Faux Pas, Beyanga, Yamba Ngai, Nairobi and Nadina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version