Connect with us

News

Mpango wa matumizi ya kawi safi Kilifi kukabili mabadiliko ya hali ya anga

Published

on

Kongamano la siku tatu kuhusu wiki ya upishi kutumia kawi safi  limezinduliwa rasmi mjini Kilifi katika kaunti ya Kilifi huku serikali kuu ikimesema inaendelea kujumuisha kila eneo katika miradi mbali mbali ya maendeleo.

Waziri wa Kawi nchini Opiyo Wandayi alisema serikali kuu inashirikisha serikali za kaunti kwenye mipango ya kawi safi ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza katika kongamano hilo, waziri Wandayi alisema Kenya inaendelea kutekeleza matumizi ya kawi safi ili kuepuka athari za kiafya kwa watumizi pamoja uharibifu wa Mazingira.

Waziri Wandayi alisistiza kuwa kwa sasa serikali inauia kuafikia utekelezaji wa sheria na mipango ya kawi safi kwa kushirikiana na wadau tofauti kwa manufaa ya jamii.

Vile vile alidokeza kuwa serikali imeitegengea kaunti ya Kilifi zaidi ya shilingi bilioni 2 zitakazotumika kuunganisha nyumba elfu 21 za ziada na nguvu za umeme.

Kwa upande wake mkewe rais Bi Rachel Ruto alisema mpango huo wa upishi safi utakomoa familia nyingi mashinani kiuchumi, kuimarisha mazingira ya elimu kwa wanafunzi majumbani vile vile kuondoa kero la wanawake katika matumizi ya mbinu za kale za upishi.

Naye gavana wa kaunti ya Kilifi Gedion Mung’aro alisema mabadiliko ya tabia nchi yamekuwa na athari kubwa kwa wakaazi hasa maeno ya Ganze na Magarini, akisistiza kuwa kawi safi pekee itaokoa maisha ya wakaazi wengi.

Mama wa taifa Bi Rachel Ruto pamoja na Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro na Waziri wa Kawi nchini Opiyo Wandayi

Ubalozi wa Uingereza na Ujerumani hapa nchini ulishinikiza serikali kukumbatia kikamilifi matumizi ya kawi safi kwa kuafikia maendeleo endelevu sawa na kubuni nafasi zaidi za ajira, kwa kushirikiana na serikali za kaunti.

Kongamano hilo linatarajiwa kukamilika alhamisi Agost 28, 2025, kauli mbiu ikiwa ni kutekeleza mikakati na mipango ya upishi safi, mabadiliko, ushirikishwaji na uwezeshaji.

Taarifa ya Joseph Jira

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

Mahakama ya Malindi yawaachilia washukiwa 3 wa kesi ya Kwa Binzaro

Published

on

By

Mahakama Kuu ya Malindi imewaachilia washukiwa watatu wanaohusishwa na kesi ya mauaji ya halaki ya watu katika kijiji cha Kwa Binzaro eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi.

Hakimu wa Mahakama hiyo Joy Wesonga aliagiza kuachiliwa huru kwa Safari Kenga Nzai, Gona Charo Kalama na Kahindi Kazungu Garama wote wakiwa wakaazi wa kijiji hicho cha Kwa Binzaro.

Watatu hao walikuwa wamekamatwa baada ya kudaiwa kuuza shamba la ekari tano kwa mshukuwa mkuu wa mauaji ya watu katika kijiji cha Kwa Binzaro Sherleen Temba Anido.

Hakimu Wesonga aliwaagiza washukiwa hao kuhakikisha wanasalimisha nakala za vitambulisha vyao vya kitaifa kwa idara husika, kuripoti kwa Naibu Chifu wa eneo hilo mara mbili kwa wiki pamoja na kujisalimisha kwa maafisa wa upelelezi wa kesi hiyo mara moja kila baada ya wiki mbili.

Miili iliyofukuliwa katika kijiji cha Kwa Binzaro 

Wakati huo huo upande wa mashtaka ukiongozwa na Naibu mkurugenzi wa mashtaka ya umma Jamie Yamina, uliomba kuwasilisha watu wengine wanne Mahakamani ikiwemo Jairus Otieno na mkewe Lilian Akinyi, Kahonzi Katana Karisa na Loise Zawadi waliojionda kama washukiwa na kugeuka kuwa mashahidi wa serikali.

Upande wa mashtaka pia uliaka kupewa siku 60 zaidi kuendelea kuzuiliwa kwa washukiwa wakuu Sherleen Temba Anido, James Kahindi Kazungu, Thomas Mukunwe na Kahidi Kazungu Garama katika kituo cha polisi cha Ngerenya, Kilifi, Watamu na Kijipwa ili kukamilisha uchunguzi wao kwani wanne hao wanakabiliwa na mashtaka ya itikadi kali, ugaidi, kujihusisha na uhalifu na kupanga mauaji.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Continue Reading

News

Chrispus aomba msahama bunge la kaunti ya Taita Taveta

Published

on

By

Mwakilishi wadi ya Bomani mjini Taveta kaunti ya Taita Taveta Chrispus Tondoo ameliomba bunge la kaunti hiyo msamaha kutokana na matamshi aliyoyatoa hapo awali akikashifu bunge hilo kwa madai ya kushamiri kwa visa vya ufisadi na utepetevu.

Tondoo akiomba msamaha katika bunge hilo alisema alitambua athari zilizosababishwa na matamshi hayo kwa wenyeji wa kaunti hiyo na bunge hilo, hali ambayo imemfanya kuchukua hatua hiyo ya kuomba msamaha.

Aidha Tondoo aliahidi kuliheshimu bunge hilo kwa mujibu wa kanuni na Sheria za bunge la kaunti ya Taita Taveta.

‘’Naomba msamaha kutokana na matamshi ambayo niliyatoa tarehe 2 na tarehe 3 mwezi wa Juni mwaka huu wa 2025 kwani hayakuwa yenye heshima kwa wenyeji wa Taita Taveta na bunge la kaunti’’, alisema Tondoo.

Tondoo alikuwa Mwakikishi wa wadi wa pili kuomba msamaha baada ya Mwakilishi wa wadi ya Kaloleni mjini Voi Ahmed Azari kuchukua hatua hiyo mwezi mmoja uliyopita.

Haya yalijiri baada ya kaimu spika wa bunge hilo Anselim Mwadime kuapa kuwachulia hatua za kisheria wanachama wanne wa bunge hilo, wawili wakiwa ni Tondoo na Azari ambayo tayari wameomba msamaha huku wawili wakiwa wamesalia bila kuomba msamaha.

Taarifa ya Janet Mumbi

Continue Reading

Trending