News
Mboko: Uongozi wa Rais Ruto haujawabagua wapwani
Mbunge wa Likoni Mishi Mboko amempongeza rais William Samoei Ruto, akisema uongozi wake haujawabagua wakaazi wa Pwani katika masuala ya maendeleo.
Akizungumza mjini Garsen katika kaunti ya Tana River, wakati wa ziara ya Naibu wa Rais Prof. Kithure Kindiki katika kaunti hiyo, Mishi alisema wataendelea kushirikiana na rais Ruto ili Pwani inufaike kimaendeleo.
Mishi pia aliwasihi viongozi na wakaazi wa Pwani kushirikiana na Rais Ruto ili kuiboresha Pwani kimaendeleo na taifa la Kenya kwa jumla.
Mishi alisema Rais Ruto ana malengo mengi na mazuri kwa taifa la Kenya na amekuwa pia akiendeleza juhudi za kuwaunganisha Wakenya ili waishi kwa umoja.
“Nasi tunasema kufa kufaana tutakufa na Daktari William Ruto, kuzama na kuzuka’’, alisema Mishi.
Mishi pia alisema utawala wa rais Ruto haujawabagua dini ya kiislamu katiwaumekuwa ikishirikisha jamii ya waislamu katika masuala mbalimbali.
Taarifa ya Janet Mumbi