Business
Mataifa yanayoshuhudia ghasia yaibua wasiwasi wa usafiri wa ndege
Kenya inapolenga kuongeza ushuru unaokusanywa katika sekta ya uchukuzi wa angani, suala la usalama wa ndege zinazosafiri kupitia mataifa yanayoshuhudia ghasia limeibua wasiwasi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya safari za ndege nchini Mary Keter alisema mabadiliko ya sera yanahitajika ili kupatia kipaumbele suala la ukaguzi na utathmini wa hatari zilizopo ili kuhakikisha ustawi hauathiri usalama au uendeshaji wa biashara.
Ikumbukwe kwamba shughuli za uchukuzi wa abiria humu nchini ziliongezeka kwa asilimia 38.5 mwaka uliopita huku wasafiri zaidi ya milioni 10 wakitumia uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta.
Haya yanajiri huku mikakati zaidi ikiendelezwa naMamlaka hiyo kuhakikisha uchukuzi wa angani unaimarika kwa asilimia kubwa licha ya changamoto za kiuchumi zinazolikumba taifa hili.
Taarifa ya Pauline Mwango