Sports

Mashindano Ya Dunia Ya Handiboli Ya Ufukweni Kuanza Rasmi Tunisia

Published

on

Kikosi cha Taifa mchezo wa Handiboli wachezaji chipukizi kuanza rasmi mashindano ya kombe la dunia hapo kesho mjini Tunis Tunisia.

Kulingana na droo iliyofanywa hii leo ni kwamba timu zote mbili upande wa wanaume na akina dada zimejumuishwa kundi B huku kikosi cha akina dada ikiratibiwa kumenyana na mataifa ya Uholanzi,Ujerumani,Rep of China kunid A zina timu za Ufaransa,Brazil,Thailand na Tanzania.

Kundi C zina timu za Tunisia,Hungary,Mexico na Senegal, Kundi la mwisho kundi D zina timu za Croatia,Uruaguay,Uhispania na Bulgaria.

Upande wa wanaume Kenya itamenyana na Hungary,Ujerumani na Tanzania huku kundi A likiwa na timu za Iran,Uhispania,Oman na Puerto Rico,Kundi C linajumuisha timu za Tunisia,Thailand,Mexico na Cook Island huku kundi D likiwa na timu Argetina,Brazil,Uruguay na Senegal.

Mashindano hayo yanaanza kesho na kukamilika Juni 22.

0 Comments

  1. Titus Kesekwa

    June 16, 2025 at 4:55 pm

    Kazi safi sana kaka na Coco tv/radio.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version