Sports

Mashemeji Debi ni Jumapili

Published

on

Mwenyekiti wa maandalizi ya CHAN mwezi Agosti nchini Nicholas Musonye amezionya vikali mashabiki wa Afc Leopards na Gor Mahia dhidi ya vurugu ya aina yoyote siku ya Jumapili Debi la Mashemeji. Kwenye kikao na wanahabari Musonye amesema iwapo viti vitangolewa au mawe kurushwa au rabsha ya aina yoyote basi vilabu hivyo vitakua hatarini.

“Viwanja vya Nyayo na Kasarani vimekarabatiwa rasmi kwa ajili ya michuano ya CHAN natoa onyo kwa mashabiki wa Afc na Gor iwapo viti vitangolewa ama Mawe kurushwa au rabsha ya aina yoyote hawatumia Tena viwanja hivi na watapata adabu Kali mno.

Vilabu hivyo viwili vinakutana kwa mara ya kwanza msimu huu mechi ya pili ikipigwa April 14 . Afc Leopards ndio wenyeji wa mechi hiyo na tayari tiketi zimeanza kuuzwa shilingi 500 mashabiki wa kawaida na 1000 mashabiki mashuhuri.Gor Mahia wako nafasi ya tatu ligini na alama 45 wakati Afc Leopards wakiwa ya Tano alama 39.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version