News

Mahakama ya Kilifi Imemhukumu Kaingu miaka 13 jela

Published

on

MAHAKAMANI-

Mahakama ya Kilifi imemhukumu kifungo cha miaka 13 gerezani mwanamume wa umri wa makamu baada ya kupatikana na hatia ya kumnajisi mtoto wa umri wa miaka 9.

Hakimu wa Mahakama ya Kilifi Ivy Wasike amesema mshukiwa Harrison Kaingu Ngolo ana muda wa siku 14 pekee wa kukata rufaa iwapo hajaridhishwa na uamuzi huo wa Mahakama.

Awali kabla ya uamuzi huo kutolewa, Mahakama imeelezwa kwamba mshukiwa alitekeleza kitendo hicho mnamo tarehe 1 mwezi Aprili mwaka 2022 katika eneo la Shingila kaunti ya Kilifi.

Mahakama pia imeelezwa kwamba mshukiwa alitekeleza unyama huo baada ya kumtuma mtoto huyo amletee maandazi kwake nyumbani ndiposa alitumia nafasi hiyo kumnyanyasa haki zake mtoto huyo.

Mahakama hata hivyo amefafanua kwamba hukumu hiyo imezingatia afya ya mtoto kwani ni miaka 3 sasa baada ya kitendo hicho, mtoto huyo bado anahisi maumivu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version