Sports

Timu Ya Taifa Ya DR Congo Yawasili Nchini Kwa Mechi Ya Ufunguzi Dhidi Ya Harambee Stars

Published

on

Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DR Congo) imewasili nchini mapema leo kwa ajili ya mechi ya ufunguzi dhidi ya Harambee Stars itakayochezwa siku ya Jumapili.

Kikosi hicho, kilicho na wachezaji 25 pamoja na benchi la kiufundi, kiliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) na kupokelewa rasmi kabla ya kuelekea hotelini jijini Nairobi.

DR Congo, maarufu kama The Leopards, ni mabingwa mara mbili wa kombe hilo na wanatarajiwa kufanya mazoezi yao ya kwanza jioni ya leo katika Uwanja wa Kasarani.

Vijana hao wako katika Kundi A pamoja na wenyeji Kenya, pamoja na AngolaMorocco, na Zambia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version