Sports
Stars Yaanza Vema Chan Kwa Ushindi Goli 1-0 Dhidi Ya DR.Congo
Timu ya Taifa ya Kenya (Harambee Stars) imechukua alama zote tatu kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwenye mchezo wa kwanza wa Kundi B wa kombe la Mataifa Afrika CHAN2024 katika dimba la Moi Sports Centre, Nairobi.
Goli hilo la kipekee lilitiwa wavuni na kiungo mshambulizi Austine Odhiambo dakika 45 kipindi cha kwanza.
Rais William Ruto ambaye alifuatilia mechi hiyo uwanjani alitembelea kikosi katika chumba cha kubadilisha na kukabidhi ahadi yake ya shilindi milioni moja kwa kila mchezaji baada ya ushindi huo.
Stars wamekwea kileleni mwa kundi A na alama Tatu kundi ambalo pia lina Morocco,Zambia na Angola Mechi ijayo ya Stars ni dhidi ya Angola ni Agosti 7.