News

LSK yashinikizwa kuwachukulia hatua Kindiki na Murkomen.

Published

on

Baadhi ya mawakili nchini wanataka chama cha mawakili nchini LSK kuwaondoa kwenye orodha ya mawakili, naibu rais Prof Kithure Kindiki na waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen.

Katika ombi lililowasilishwa kwa chama hicho, mawakili hao wakiongozwa na Wakili Kepha Ojijo, walisema licha ya viongozi hao wawili kuwa walimu wa sheria walikiuka sheria wakati wa maandamano.

Ombi hilo pia liliwashutumu wawili hao kwa utovu wa nidhamu huku wakili Ojijo akisema Kindiki na Murkomen wakati wakihudumu kwenye idara ya usalama, walisimamia oparesheni za polisi ambazo zilisababisha vifo, majeruhi na utekaji nyara kati ya mwaka wa 2024 na 2025.

Wakili Ojijo, alitaka kuwepo na kikao maalum na cha dharura cha wanachama wa LSK ili kupiga kura ya iwapo watawaondoa wawili hao kwenye orodha ya mawakili nchini ama suala hilo lipelekwe kwenye mahakama ya nidhamu ya mawakili.

Kauli yake ilijiri wakati ambapo serikali imeonekana ikikiuka sheria wakati wa maandamano yaliyoongozwa na vijana wa Gen Z huku mashirika ya kutetea haki za kibinadamu nchini yakiishtumu serikali kwa kutumia nguvu kupita kiasi wakati wa kukabiliana na waandamanaji.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version