Sports
Ligi Limetuponyoka Asema Zico
Mkufunzi wa Kilabu ya Gor Mahia Zedekiah Zico Otieno amekubali kwamba ligi imewaponyoka baada ya kutoka sare na kilabu ya Afc Leopards ugani raila odinga katika debi la Mashemeji jana jioni.
Kiungo matata Austine Odhiambo aliweka uongozini Kogalo kipindi cha kwanza dakika ya 30 kabila ya Brian wanyama kuisawazishia chui dakika ya 55 kipindi cha pili na kocha huyo anaamini taji limewatoka baada ya sare hiyo inayowacha nafasi ya tatu.
“Tulianza Vizuri lakini concetration lapse imetucost kipindi cha pili,lengo letu lilikua kupata ushindi hapa ili kuweka pressure kwa viongozi lakini sasa matokeo haya ni ishara tosha sasa itabidi tuangazie taji la Mozzartbet Cup.”
Kwa upande wake Mkufunzi wa Afc Leopards Fred Ambani amesema kwamba ameridhishwa na matokeo hayo akijigamba angali kupoteza mechi ya Debi akiwa mchezaji na sasa kama kocha wa Ingwe.
“Vijana walioanza mechi kwa mchecheto na uoga mwingi katika kipindi cha kwanza ila tulipoenda katia dressing room nikawambia watulie na ndiposa tukarejea mchezoni,ningali kupoteza debi kama mchezaji sikuwahi na sasa kama kocha pia bado sijapoteza.
Gor inasalia ya tatu na alama 55 huku Afc Leopards wakibaki ya sita na alama 47.