Sports
Ligi Limetuponyoka Asema Zico

Mkufunzi wa Kilabu ya Gor Mahia Zedekiah Zico Otieno amekubali kwamba ligi imewaponyoka baada ya kutoka sare na kilabu ya Afc Leopards ugani raila odinga katika debi la Mashemeji jana jioni.
Kiungo matata Austine Odhiambo aliweka uongozini Kogalo kipindi cha kwanza dakika ya 30 kabila ya Brian wanyama kuisawazishia chui dakika ya 55 kipindi cha pili na kocha huyo anaamini taji limewatoka baada ya sare hiyo inayowacha nafasi ya tatu.
“Tulianza Vizuri lakini concetration lapse imetucost kipindi cha pili,lengo letu lilikua kupata ushindi hapa ili kuweka pressure kwa viongozi lakini sasa matokeo haya ni ishara tosha sasa itabidi tuangazie taji la Mozzartbet Cup.”
Kwa upande wake Mkufunzi wa Afc Leopards Fred Ambani amesema kwamba ameridhishwa na matokeo hayo akijigamba angali kupoteza mechi ya Debi akiwa mchezaji na sasa kama kocha wa Ingwe.
“Vijana walioanza mechi kwa mchecheto na uoga mwingi katika kipindi cha kwanza ila tulipoenda katia dressing room nikawambia watulie na ndiposa tukarejea mchezoni,ningali kupoteza debi kama mchezaji sikuwahi na sasa kama kocha pia bado sijapoteza.
Gor inasalia ya tatu na alama 55 huku Afc Leopards wakibaki ya sita na alama 47.
Sports
Timu Ya Taifa Ya DR Congo Yawasili Nchini Kwa Mechi Ya Ufunguzi Dhidi Ya Harambee Stars

Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DR Congo) imewasili nchini mapema leo kwa ajili ya mechi ya ufunguzi dhidi ya Harambee Stars itakayochezwa siku ya Jumapili.
Kikosi hicho, kilicho na wachezaji 25 pamoja na benchi la kiufundi, kiliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) na kupokelewa rasmi kabla ya kuelekea hotelini jijini Nairobi.
DR Congo, maarufu kama The Leopards, ni mabingwa mara mbili wa kombe hilo na wanatarajiwa kufanya mazoezi yao ya kwanza jioni ya leo katika Uwanja wa Kasarani.
Vijana hao wako katika Kundi A pamoja na wenyeji Kenya, pamoja na Angola, Morocco, na Zambia.
Sports
Waziri Wa Michezo Salim Mvurya Asema Kenya Iko Tayari Kwa CHAN

Waziri Mvurya, akizungumza katika Uwanja wa Nyayo, amesema kuwa fursa hiyo ni ya kipekee kwa taifa na sekta ya michezo kwa ujumla, huku maandalizi ya kuelekea AFCON 2027 yakiendelea.
Aidha, Mvurya amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kushangilia timu ya taifa, Harambee Stars, katika mechi ya Jumapili na michezo yote ya michuano hiyo.
Harambee Stars itacheza mechi zake zote katika Uwanja wa Kasarani. Timu hiyo imo katika Kundi A pamoja na Angola, Morocco, Zambia, na DR Congo.