Business
Kufungwa kwa Shule Kwaathiri Mapato ya Bodaboda
Wahudumu wa bodoboda kutoka eneo la Kibaoni kaunti ya kilifi wanasema kuwa biashara hiyo imedorora baada ya wanafunzi kufunga shule kwa likizo fupi.
Kulingana na Robert ngala biashara hiyo inategemea zaidi wanafunzi, na hatua ya shule kufungwa kumefanya biashara hiyo kuyumba.
Wakizungumza na meza yetu ya biashara Ngala anasema kuwa kwa sasa wateja wamepungua hali iinayowaathiri kiuchumi.
Aidha ngala ameongeza kuwa mara kwa mara wamelazimika kupunguza hata kiwango cha nauli ili kuhakikisha kuwa wanapata riziki ya siku.