Sports
Twende Kasarani Tushabikie Stars- Asema Waziri Mvurya
Waziri wa michezo Salim Mvurya ametangaza kwamba matayarisho ya michuano ya CHAN yamekamilika na vijana wa nyumbani wako tayari kuakilisha Taifa.
Kenya itatumia viwanja vya Kasarani, na Nyayo, huku viwanja vya Polisi SACCO, Kasarani Annex na Ulinzi sports Complex, vikitumika Kwa mazoezi ya timu zote zinazoshiriki michuanobuii.
Akizungumza mjini Kilifi, Waziri Mvurya aliwahakikishia Wakenya burudani huku akiwaalika kujitokeza Kwa wingi kushabikia timu ya Taifa Harambee Stats.
Ukarabati wa Viwanja hivi viwili umekamilika hivi majuzi na kukabidhiwa rasmi Kwa Kamati andalizi ya michuano hiyo kwenye hafla iliyohudhuriwa na Waziri wa Usalama Kipichunba Murkomen na Waziri Mvurya.
Timu ya Taifa Harambee stars itafungua dimba hilo ikiwa katika Kundi A pamoja na DR Congo, Morocco, Zambia na Angola. Kundi hili kimetajwa kuwa gumu zaidi.