Sports

Kiungo Wa Brenford Bryan Mbeumo Sasa Ni Mali Ya United

Published

on

Baada ya vute ni kuvute ambayo imedumu kwa kipindi cha mwezi mmoja ni rasmi kwamba kilabu ya manchester United na Brenford wameafikia makubaliano ya pauni milioni 70 ya kiungo mshambulizi Bryan Mbeumo raia wa Cameroon.

Haya yanajiri baada ya ofa mara mbili ya united kukataliwa na kilabu hio kabila ya kutuma ofa ya mwisho ya pauni milioni 65 na nyongesa ya pauni milioni 5.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 yuko tayari kumwaga wino mkataba wa miaka mitano baada kukubali matakwa yake binafsi.

Mbeumo anakua sajili wa pili kwa kocha mkuu Ruben Amorim baada ya ujio wa mshmabulizi Matheus Cunha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version