Sports
Kocha Wa Stars Benni McCarthy Atoa Sababu Ya Kujiondoa CECAFA

Mkufunzi wa Timu ya Taifa ya Soka Harambee Stars Benni McCarthy amesema kwamba walienda Tanzania kushiriki Kombe la CECAFA wakiwa na azma na ari kubwa ya kuhahakisha wanajiandaa vyema kwa taji la Chan mwezi Ujao ila mandhari waliokutana nayo hayakua ya kuridhisha ndipo wakafikia makubaliano ya kurejea nchini.
Akizungumza kwa mara ya kwanza vijana wa nyumbani wakizidi kujinoa Ugani Nyayo mwalimu huyo amekiri mortisha iliku juu mno ila mazingira hayo hayangeruhusu wao kufanya Kazi na kujianda Ugani Karatu Arusha. “Tuliketi chini kama benchi la Kiufundi tukaona ubora wa viwanja vya mazoezi na wa michezo tukaona itakua si salama kwa wachezaji kuelekea CHAN hivyo tukarejea”.
Haya yanajiri baada ya stars kujiondoa kwenye kipute Cha CECAFA Cha Mataifa Manne nchini Tanzania siku ya Jumatatu huku maswali chungu nzima yakibaki vinywani mwa wengi.
Hata hivyo mwalimu huyo anasema kwa sasa wanajitayarisha zaidi kwa Kombe Hilo kwani wanajua fika ugumu wa kundi lao.
Stars wako KUNDI A pamoja na Angola, Morocco, Zambia na DR.Congo.
Continue Reading
Sports
Tuko Tayari Kwa CHAN Asema Kocha Wa Angola-Pedro

SIKU 9 KUNGOA NANGA KWA CHAN
ANGOLA-Mabingwa wa Taji La COSAFA.
Wanajiita The Black Antelopes kwa jina la utani ila bado hawajashinda kombe la CHAN katika historia yao.
Taifa hilo limeshiriki kombe hilo miaka minne ikiwa ni miaka ya (2011, 2016, 2018, 2022) zote wakiambulia patupu.
Kocha mkuu wa timu hiyo ya taifa anaitwa Pedro Gonçalves ambaye ameongoza timu za taifa hilo kuanzia kwa vikosi chipukizi wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 taji la AFCON NA COSAFA ya chipukizi kabila ya kuongoza taifa hilo kushinda kombe la COSAFA wakishinda Afrika Kuisini magoli 3-0 kwenye fainali mwezi jana.
Akizungumza kabila ya timu hiyo kuwasili jijini Nairobi mwalimu huyo amesema lengo lao ni kuendeleza walipoachia ; “Tumefanya vizuri sana Cosafa na sasa lengo letu kushinda Chan pia nina kikosi ambacho kiko tayari na tutafanya kila kitu kuibuka washindi.”
Mwalimu huyo pia ameongoza taifa lake katika kombe la AFCON mwaka 2024 wakitolewa kwenye robo fainali nchini Ivory Coast.
The Sable Antelopes ilimaliza nafasi ya nne taji la Chan katika fainali ya mwaka 2011 nchini Sudan.
Badhi ya wachezaji wa kuangaziwa katika kikosi cha vijana hao ni pamoja na ;mshambulizi Jó Paciência wa kilabu ya Bravos do Maquis nchini humo mabeki Eddie Afonso na Hossi.
Mabingwa hao wa COSAFA wako kundi A pamoja na Kenya,Morocco,DR.Congo na Zambia.
Sports
Finali Ya Euro Ya Akina Dada Ni Kati Ya Uhispania Na Uingereza Jumapili

Timu ya Taifa ya Wanawake ya Uhispania imetinga fainali ya kombe la Mataifa ya Ulaya kwa Wanawake mwaka 2025, WEURO 2025 kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Ujerumani katika dimba la Letzigrund mjini, Zürich kwenye nusu fainali.
Timu zote mbili zilikosa nafasi kochokocho za kufunga katika mchezo huo huku Uhispania wakilenga zaidi ya mashuti 10 langoni ila haikuzaa matunda katika dakika 90 za mchezo.
Mchezo huo ulilazimika kuamuliwa kwenye muda wa ziada ambapo mshambulizi wa Barcelona Aitana Bonmati alifunga goli la kipekee dakika ya 113 baada ya dakika 90 kumalizika bila bao.
Uhispania itachuana na Mabingwa watetezi, England kwenye fainali siku ya Jumapili.
England waliwabandua Italia magoli 2-1 katika nusu fainali ya kwanza siku ya Jumanne.