Sports
Kilabu Ya Barca Kurejea Camp Nou Agosti
Ni rasmi kuwa kilabu ya Barcelona ya Uhispania itarejea kwenye uga wao wa kihistoria Camp Nou Agosti 10 kwa ajili ya Kombe la Joan Gamper, mchuano wao wa Ufunguzi wa msimu.
Uwanja huo umekua ukikarabatiwa kwa muda wa misimu miwili sasa ikiwalazimu miamba hao wa Catalunya kuutumia uwanja wa Olympic stadium kwa kipindi hicho katika mechi zake zote.
Barca hata hivyo itacheza mechi za nyumbani na mashabiki kati ya 50,000 hadi 60,000 kwanza mpaka pale itakapokamilisha kikamilifu ukarabati na utaweza kuhifadhi mashabiki 99,354
Mara ya mwisho Barcelona kucheza Camp Nou ilikuwa Mei 2023.