Sports
Kikosi Cha Taifa Mchezo Wa Netiboli Yashinda Shaba-UAE
Kikosi cha Taifa kwa akina dada mchezo wa Pete marufu kama Divas waliweza kumaliza ya tatu na kushinda tuzo la Shaba katika mashindano ya UAE Netball Championship katika milki za kiarabu.
Vipusa hao walishinda mechi ya mwisho alama 46-37 dhidi ya Ireland na kupata nishani hiyo ya shaba.
Taifa La Namibia liliweza kuwangusha mibabe na kushinda kombe hilo na tuzo la Dhahabu mechi ya mwisho kwa alama 62-53 dhidi ya taifa la Singapore.