Entertainment
Kelechi: Kama Content Haibebi Bila Mimi, Rethink the Plan – Clout Si Career
Kelechi Afrikana, kwa mara nyingine tena ametoa ujumbe mzito kwa wale wanaotafuta umaarufu (clout) kupitia jina lake, akisisitiza kuwa muziki unapaswa kuwa msingi wa mafanikio ya kweli – si kelele za mitandaoni.
Kupitia chapisho kwenye Facebook, Kelechi alitoa kauli kali iliyogusa si tu maisha ya wasanii, bali pia maudhui ya mitandaoni yanayozidi kutawaliwa na mbinu za kuvutia macho badala ya vipaji halisi.
Wasanii wengi wamekuwa wakikumbana na wimbi la “drag culture” – watu wanaotengeneza maudhui kwa kumhusisha na kumchafua bila sababu, ili kuvutia wafuasi au kuteka macho ya mtandao lakini Kelechi ameweka wazi kwamba kuvuma si sawa na kustahimili, na mafanikio ya kweli yanatokana na kazi halisi, si drama ya kupangwa.
“Si lazima utaje jina yangu ndo upate followers bruv 😤 Clout si career — especially when you’re forcing it off someone else’s wave. Kama content haibebi bila kudrag jina ya mtu, maybe it’s time to rethink the whole plan,” Kelechi alisema.
Kelechi aliwakumbusha wafuasi wake kuwa muziki ni sanaa — na kama kazi yako haiwezi kujisimamia bila kuchomeka jina la mtu mwingine, basi kuna haja ya kutathmini upya dhamira yako.
Post ya Kelechi ilikuwa pia ya shukrani na matumaini. Kelechi aliwashukuru mashabiki wake na hasa @mummiefrancie, kwa kuonyesha upendo mkubwa kwa wimbo wake mpya “Litapita”.
Aliandika: “Mkinisisupport walai naeza fika mbali 🙏🔥 Shukran sana @mummiefrancie Francie kwa kuvybea na kuonyesha upendo kwa ngoma yangu “Litapita” 🥹❤️Support kama hii inanipa nguvu ya kuendelea, na najua naweza go far with y’all behind me!”
Chapisho la Kelechi ni zaidi ya rant ya mtandao – ni tamko la msanii anayeamini katika kazi yake, anayetaka kuona muziki wake ukithaminiwa kwa ubora wake, si kwa kiki.
Ikumbukwe kuwa baadhi ya wasanii wamekuwa wakitumia kiki kusukuma kazi zao. Hata hivyo, Kelechi anatufundisha thamani ya vitu vya kweli: kazi, maadili, na kuaminiana.
Kelechi alisema: “Let the music speak — not the noise.” 🎧🚫