Business
Kaunti ya Mombasa kuwekeza fedha za kazi kwa vijana
Serikali ya kaunti ya Mombasa inalenga kuwekeza shilingi laki moja ili kunufaisha miradi ya mafunzo na ajira kwa vijana kujiendeleza kimaisha.
Katibu katika Wizara ya biashara, utalii na utamaduni kaunti ya Mombasa, Hamisi Juma Kurichwa, alisema serikali ya kaunti kwa ushirikiano na benki ya KCB, ambayo pia itatoa shiling laki moja.
Aidha alieleza kwamba fedha hizo zitatumika kama mtaji kwa vijana kuinua makundi yao.
Mpango huu unalenga kuwawezesha vijana kuanzisha biashara ndogondogo ili kujitegemea kimaisha na kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira.
Wakati huo huo alisema utekelezaji wa mpango huu utaanza rasmi baada ya bunge la kaunti ya Mombasa kuidhinisha hazina ya Revolving Fund, ambapo zaidi ya vijana elfu kumi wanatarajiwa kunufaika na mpango huo.
Taarifa ya Pauline Mwango