Sports
Kasarani Na Nyayo:Uwezo Wa Kubeba Mashabiki Yapungua
CHAN Siku 17 zimesalia kipute hicho kungoa nanga nchi za Kenya,Uganda na Tanzania.
Serikali ya Kenya kupitia Wizara ya Michezo imetumia Kima Cha zaidi ya Shilingi Bilioni 6.7 kufanyia Ukarabati uwanja wa Kasarani na Shilingi nyingine Bilioni 1.1 Uga wa Nyayo.
Uwanja wa Kasarani Ulifungwa mwaka 2023 Kwa shughuli hiyo ya ukarabati huku uga wa Nyayo ukifungwa mwaka mmoja badaye 2024 kwa Maandalizi ya kipute cha CHAN kinachotarajiwa kung’oa nanga chini ya siku 17 zijazo.
Viwanja hivyo sasa vinauwezo wa kubeba mashabiki 55,000 na 22,000 mtawalia.
Ikumbukwe kabila ya ukarabati wa uwanja wa Kasarani ulikuwa na uwezo wa kuwabeba takriban mashabiki 60,000 huku uwanja wa Nyayo ukibeba mashabiki 30,000.