Sports
Harambee Stars Yazidi Kujinoa Morocco
Timu ya taifa Harambee Stars imefanya mazoezi ya kwanza nchini Morocco inapojiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Chad hapo kesho.
Vijana wa nyumbani waliwasili nchini humo chini ya kocha Benni McCarthy ambaye ameelezea kwamba kwa sasa anajenga kikosi chenye ubora zaidi kwa siku za usoni
“Ni muda bora mimi kuwajua wachezaji wangu kwani hatujakua pamoja tangu mechi za kufuzu kombe la dunia dhidi ya Gambia na vile vile Gabon,wachezaji niliowaita ni sura ya timu ambayo naiunda si tu kwa Chan bali pia Afcon mwaka 2027 nchini.”
Stars hata hivyo waliwasili bila wachezaji mahiri akiwemo mshambulizi nyota Michael Olunga,kiungo Duke Abuya,Masud Juma,John Ayunga miongoni mwa wnegine kwani bado wako kwenye majukumu ya vilabu vyao ligi za nyumbani.
Timu hiyo inashuka dimbani dhidi ya Chad Juni 6 na Juni 10.