Sports

Fikirini Jacobs- Benni Mccarthy Ni Sahihi Harambee Stars

Published

on

Katibu katika Wizara Kuu ya Kitaifa Inayosimamia Maswala ya Vijana na Uchumi Bunifu Fikirini Jacobs amesifia hatua ya Shirikisho la soka nchini FKF na serikali kupitia kwa Wizara ya Michezo kumteua Benni Mccarthy kuwa kocha mkuu wa timu ya soka wanaume Harambee Stars.

Kwa mujibu wa Katibu huyo hatua hiyo ni ishara tosha ya kufufuka kwa mchezo huo nchini baada ya ukimya wa muda mrefu kwenye timu hiyo.

“Nichukue Fursa Hii kuwapongeza Wizara ya Michezo ambapo yuko mwenzangu Elijah Mwangi sitaki nizungumz mengi lakini hata hatua ya Taifa La Kenya kumchukua Benni Mccarthy aliyekua kocha Manchester United kuwa kocha wa Harambee Stars ni hatua ya kufufua timu hiyo pamoja na The Lost Glory ,kwa sababu kihistoria mimi ni mtu nimekaa na watu wengi akiwemo mzee wetu The RT HON.Raila Amollo Odinga na aliwahi kuniambia hapa kenya mpira ulikua mkubwa mno kuliko magharibi na hata Afrika Kusini.”

Katibu huyo aliyasema hayo katika fainali ya mashindano ya kaunti ya shule za Upili katika shule ya Upili ya kilifi towship.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version