News

Erastus Edung Ethekon Aapishwa Kuwa Mwenyekiti Mpya wa Tume Ya IEBC

Published

on

Wenyekiti mpya wa Tume ya uchaguzi na mipaka Erastus Ethekon pamoja na makamishena wengine sita wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), wameapishwa leo Ijumaa Julai 11 katika jengo la Mahakama ya upeo.

Mwenyekiti huyo sasa atawaongoza makamishena wengine, Ann Nderitu, Moses Mukhwana, Mary Sorobit, Hassan Noor, Francis Adoul, na Fahima Abdallah kuhudumu katika time hiyo.

Awali zoezi la kuwapishwa makamishena hao, lilikuwa limesimamishwa kufuatia agizo la Mahakama kuu, iliyotaja ukiukwaji mkubwa wakati wa mchakato wa kuwateua makamishena hao.

Hata hivyo agizo hilo sasa limeondolewa na majina ya makamishena hao kuchapishwa upya katika gazeti rasmi la serikali hapo Jana Julai 10 2025.

Mnamo Julai 10 2025, Mahakama kuu ilikuwa imebatlisha uteuzi uliofanywa na Rais William Ruto wa Makamishena hao saba wa tume ya uchaguzi na mipaka (IEBC), akiwemo mwenyekiti wake Erastus Ethekon.

Hata hivyo katika uamuzi huo, Mahakama ilimpa nafasi Rais William Ruto kuhalalisha uteuzi wa makamishena hao kwa kuondolewa mbali kwa agizo hilo la awali lililozuia kuchapishwa kwa majina ya makamishena hao katika gazeti rasmi la serikali kabla ya kula kiapo.

Katika uamuzi wao siku ya Alhamisi Julai 10 2025, majaji wa Mahakama hiyo Roseline Amburili, Jaji Bahati Mwamuye na John Chigiti, walisema kwamba Rais alipasa kuheshimu maagizo hayo ya Mahakama kwani si mapendekezo tu, bali yalikuwa na msingi wa kisheria na kuapishwa kwa Makamishena hao ungekuwa kinyume Cha Sheria, na kuwatoa imani Wakenya kwa Tume hiyo.

Tume hiyo sasa inajukumu kubwa la kushughulikia masuala nyeti yaliyokuwa yamekwama tangu kuvunjwa kwa tume iliyokuwa iliongozwa na Wafula Chebukati.

Miongoni mwayo ni chaguzi ndogo katika sehemu mbali mbali za uakilishi Wadi na Ubunge likiwemo eneo Bunge la Magarini Kaunti ya Kilifi.

Pia kuna suala la kusafisha sajili ya wapiga kura pamoja na kuchunguzwa upya kwa mipaka ya maeneo ya kiwakilishi kabla ya uchaguzi mkuu ujao wa 2027.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version