Business
Sekta ya Uchukuzi Yatikiswa na Kupanda kwa Bei ya Mafuta
Sekta ya uchukuzi huenda ikaathirika hata zaidi baada ya mamlaka ya kudhibiti kawi nchini kuongeza bei ya mafuta ya petrol , disel na mafuta ya taa.
Kulingana na wahudumu wa matatu,tuktuk na bodaboda kutoka kaloleni kaunti ya kilifi bei mpya ya mafuta ambayo imetangazwa na mamlaka hiyo ,huenda ikawazaimu kupandisha nauli ili kukuendelea kujikimu kimaisha.
Aidha wahudumu hao wamesema hatua hiyo huenda ikasababisha kudorora kwa biashara kwani wateja wengi watalazimika kutembea kwa miguuu hali ambayo itafanya maisha kuwa magumu .
Wakizungumza na cocofm wahudumu wa boda boda wameikosoa serikali kwa kushindwa kupunguza gharama ya maisha jinsi walivyoahidi wakati wa kampeini.
Wakati huo huo wafanyabiashara wadogo wadogo katika eneo hilo wameeleza wasiwasi wao kuhusu kupanda kwa bei hizo hasa wanaotegemea mafuta ya taa wakisema maisha yatakuwa magumu zaidi.