Sports

Djokovic Kuzipiga Na Sinner Nusu Fainali Ya Tennis Mjini Wimbledon

Published

on

Matumani ya bingwa wa mpira wa Tennis Novak Djokovic kupata taji la 25 la Grand slam katika historia ya mchezo huo yangali hai anaposhuka dimbani kwa Nusu fainali dhidi ya mchezaji anayeorodheshwa wa kwanza ulimwenguni kwa sasa Jannik Sinner.

Raia huyo wa Serbia alijitosa kwenye awamu hiyo kwa kushinda Flavio Cobolli raia wa Marekani kwa seti za  6-7 (6/8), 6-2, 7-5, 6-4 katika awamu ya robo fainali mbele ya malkia wa Britain Camila.

Kwa upande wake mchezaji namba moja Jannik Sinner alimpiku mwenzake Ben Shelton raia wa Marekani anayeorodheshwa wa 10 ulimwenguni kwa seti za 7-6 (7/2), 6-4, 6-4.

Katika Nusu fainali ya pili mchezaji anayeorodheshwa wa pili ulimwenguni Carlos Alcaraz kuzipiga dhidi ya Taylor Fritz raia wa marekani.

Upande wa akina dada mwanadada anayeorodheshwa wa kwanza ulimwenguni Aryna Sabalenka atajitosa ugani kucheza dhidi ya Amanda Anisimova raia wa Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version