News

Daraja la Sabaki kwenye hatari ya kuporomoka

Published

on

Daraja la Sabaki eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi limo hatarini ya kuporomoka kufuatia mvua kubwa inayoendelea kuonyesha katika kanda ya Pwani na kusababisha mmomonyoko wa udongo mkabala na daraja hilo.

Mmomonyoko huo sasa yamesababisha ufa mkubwa kwa upande mmoja wa daraja hilo la Sabaki hali inayozidi kuwatia hofu watumiaji wa kivuko hicho.

Wasafiri wanatumia magari kuvuka daraja hilo hawana ufahamu wa hatari hiyo kwani kufikia sasa daraja hilo halijaathiriwa na mmomonyoko huo ambao usipodhibitiwa mapema huenda ukaliacha daraja hilo likining’inia upande mmoja kama mvua itaendelea kunyesha.

Wakaazi wa eneo la Sabaki wameelezea wasiwasi wao, japo tayari mafundi kutoka idara ya ujenzi wanatarajiwa kufika katika sehemu hiyo ili kurekebisha hali hiyo.

Ikumbukwe kwamba eneo hilo lina historia ya mikasa kwani mnamo Aprili 2, 2001 zaidi ya watu 50 walipoteza maisha yao katika mkasa wa mabasi mawili yalipogongana na kutumbukia kwenye mlango wa moto Sabaki unaomwaga maji bahari hindi.

Daraja hilo lina umuhimu mkubwa na linaunganisha kaunti za Kilifi, Tana River na Lamu katika sehemu hiyo ambayo mto Sabaki unakaribia kuingia katika bahari hindi.

Taarifa ya Lolani Kalu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version