News
Daktari Sudi, ahimiza wanaume kuzingatia mbinu za kupanga uzazi
Daktari wa Afya ya uzazi katika hospitali ya Malindi kaunti ya Kilifi, Sudi Mohamed amewashinikiza wanaume katika eneo bunge la Malindi na kaunti ya Kilifi kwa jumla kuzingatia mbinu za kisasa za upangaji uzazi.
Akizungumza na Mwanahabari wetu hospitalini humo, Daktari Mohamed amesema mbinu hizo hazina madhara yoyote kwa afya ya uzazi ya wanaume.
Daktari Mohamed ameitaka jamii kuondoa dhana potofu kuhusu mbinu hizo za upangaji.
Wakati huo huo Daktari Mohamed amesema ikiwa wanaume watazingatia mbinu za upangaji uzazi itakuwa vyema kwao kwani zitawaepusha wake wao dhidi ya madhara yanayotokana na utumizi wa mbinu za upangaji uzazi.
Taarifa ya Janet Mumbi