Health

Eneo la Rabia linaongoza kwa idadi ya watoto ambao hawajapokea chanjo

Published

on

Eneo la Rabai kaunti ya Kilifi ndio eneo linaloongoza katika kaunti nzima ya Kilifi na idadi kubwa ya watoto ambao hawajapokea chanjo yoyote inayochanjwa watoto.

Haya ni kwa mujibu ya takwimu za afya kutoka kwa idara inayoshughulikiwa masuala ya chanjo katika kaunti ya Kilifi.

Muuguzi msimamizi wa masuala ya chanjo katika kaunti ya Kilifi, Christine Mataza alisema kufikia mwezi wa saba ni asilimia 36 pekee ya watoto wote kaunti ya Kilifi ambao walipokea chanjo.

Christine alisema kuwa kupitia warsha hiyo na wadau mbalimbali wakijumuisha viongozi wa kidini, mashirika na viongozi wa kijamii wamekubaliana kuimarisha hamasa mashinani kuhusiana na umuhimu wa wazazi kuwapeleka watoto wao kupata chanjo

Muuguzi msimamizi wa masuala ya chanjo katika kaunti ya Kilifi, Christine Mataza

Aidha aliwahimiza wakaazi wa Kilifi kuzingatia hamasa hizo zitakazowafikia kupitia wadau mbalimbali ili watoto wao wapate chanjo akieleza kuwa ukiukaji wa baadhi ya chanjo huenda ukamsababishia mtoto ulemavu wa kudumu

Kwa upande wake msimamizi wa afya ya jamii kaunti ya Kilifi, Amos Ndenge aliitaja mikakati ambayo wameweka kuhakikisha kuwa wanafikia malengo yaliyowekwa kufungamana na idadi ya chanjo.

Viongozi wa kidini waliohudhuria warsha hiyo waliahidi kushirikiana ili kuafikia malengo ya idara hiyo ya chanjo.

Taarifa ya Hamis Kombe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version