Sports

CAF Imepiga Tiki Kenya Kuanda CHAN – Musonye

Published

on

Shirikisho la soka Barani Afrika CAF limetupa idhini kuandaa chan haya si maneno yangu bali ya mwenyekiti wa kamati andalizi ya CHAN Nicholas Musonye.

Akizungumza na vyombo vya habari mapema leo Musonye amesema kwamba CAF wamepiga tiki kenya kwa maandalizi ya kombe hilo badaye mwezi ujao uwanjani Kasarani.

“Shirikisho la Soka CAF lina imani nasi na hivyo limetupa nafasi ya kuanda taji la CHAN mwezi ujao,kwa sasa tunaomba watu wa nchi hii na Afrika Mashariki kwa jumla waje wafurahiye mchezo wa Soka Nairobi.”

Pia Musonye amefichua kwamba kiingilio ya mechi hizo ni kama ifuatayo;

Mashabiki mashuhuri zaidi shs.1000,mshabiki Mashuhuri kulipia ada ya shilingi 500 nao wa Russia kulipia shilingi 200.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version