Wakulima wa mapapai kutoka eneo bunge la Ganze kaunti ya Kilifi wameitaka serikali ya kaunti kwa ushirikiano na serikali kuu kujenga viwanda ili kuwasaidia kuuza matunda yao.
Wakizungumza na cocofm wakulima hao walisema kuwa msimu huu mapapai ni mengi japo wateja ni wachache mno, hali ambayo inafanya matunda hayo kuharibika sokoni.
Kulingana na wakulima hao, wanakadiria hasara kwani mapapai yanaoza mashambani kutokana na ukosefu wa soko.
Walisema iwapo serikali itawatengeneza kiwanda cha matunda kaunti ya Kilifi basi huenda uchumi wao ukainuka na kuwapatia motisha wa kundeleza kilimo hicho.
Ni kauli ambayo iliungwa mkono na wafanyibiashara wa matunda katika soko la Kwa Charo wa Mae ambao walisema kuwa wanakadiria hasara kutokana na mapapai kuharibika sokoni kutokana na wingi wa matunda hayo.
“Mapapai sai ni mengi mashambani na hakuna soko hali ambayo inafanya matunda kuharibika shambani, serikali inafaa kujenga viwanda ili kutusaidia kuuza matunda ili kutupunguzia hasara hizi tunazopata.”walisema wakulima.
Taarifa ya Pauline Mwango.
