Idara ya hali ya hewa nchini yaonya kuhusu mvua mkubwa

Idara ya hali ya hewa nchini yaonya kuhusu mvua mkubwa

Idara ya hali ya hewa nchini imeonya kuwa mvua za wastani hadi mvua nyingi zinatarajiwa kunyesha katika baadhi ya maeneo ya Nairobi na kaunti jirani katika saa 24 zijazo.

Katika taarifa yake idara hiyo imesema mvua hizo zitaathiri hasa maeneo ya nyanda za juu mashariki mwa Bonde la Ufa, ikiwemo Kaunti ya Nairobi.

Kulingana na utabiri huo, hali ya mawingu inatarajiwa asubuhi ya leo kabla ya kupisha vipindi vya jua, huku kukiwa na uwezekano wa mvua nyepesi katika maeneo ya nyanda za juu.

Kaunti za pwani, zikiwemo kaunti ya Mombasa, Kwale, Kilifi, Lamuna Tana River, zinatarajiwa kupata manyunyu mepesi ya mvua, huku mvua zaidi zikitarajiwa asubuhi ya leo na alasiri, hasa katika pwani ya kusini.

Utabiri huo pia umeonya kuhusu upepo mkali wa kusini mashariki unaozidi mafundo 25katika baadhi ya maeneo ya Kaunti ya Turkana na Kaunti ya Marsabit.

Taarifa ya Joseph Jira