Mwenyekiti wa Bodi ya hazina ya michezo, sanaa na maendeleo Wakili George Kithi amesisitiza umuhimu wa viongozi kuwaelimishwa wananchi kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali mashinani.
Wakili Kithi alisema wananchi wengi bado hawana ufahamu wa kutosha kuhusu miradi hiyo na jinsi inavyowanufaisha, hali inayochangia kutokuelewa juhudi zinazofanywa na serikali.
Aidha aliongeza kwamba kaunti za Pwani ni miongoni mwa kaunti zilizopata manufaa makubwa kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo katika serikali, tofauti na ilivyokuwa katika utawala uliopita.
“Ni muhimu kwa viongozi kujieleza kwa wananchi kuhusu miradi ya maendeleo iliyofanywa na ambayo itafanywa kwa sababu mwananchi hana ufahamu, kwa mtu wa Kilifi ni muhimu kwa Wananchi aelewe kwamba serikali inamjali na kwa malengo gani, jukumu hilo liko chini ya viongozi kuwaeleza wananchi”, alisema Wakili Kithi.
Wakati huo huo, aliwahimiza wananchi kuwa na uvumilivu na kuipa serikali nafasi ya kutosha ili kutekeleza kikamilifu mipango yake ya maendeleo kwa kwa wananchi.
Taarifa ya Mwanahabari wetu
