Washikadau wa sekta ya elimu nchini kwa ushirikiano na wataalamu wa masuala ya maendeleo wamezindua mkakati wa ruwaza ya mwaka 2040, kuboresha sekta ya elimu.
Wakiongozwa na Shirika la Mizizi Elimu Afrika, wamesema hatua hiyo ya mda mrefu, inalenga kuimarisha misingi bora ya elimu katika bara la Afrika
Wakizungumza jijini Nairobi, washkadau hao wa sekta ya elimu nchini wamesisitiza haja ya ushirikiano kati ya serikali na sekta za kibinafsi ili kuhakikisha watoto na vijana wanapata elimu bora na yenye usawa.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Mizizi Elimu Afrika John Mugo alisema suluhu la mda mrefu utazikabili changamoto zinawakumba wanafunzi.
“Mkakati huo uko na malengo bora kwa wanafunzi kwani unalenga kuwawezesha wanapata elimu bora na yenye usawa”, alisema Mugo.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi
