Serikali imesema imeweka mipango ya kuimarisha ufugaji mashiani kupitia teknolojia ili kupiga jeki uchumi wa taifa.
Akizungumza nchini Qatar rais Wiliam Ruto alisema kuwa ufugaji ni kiungo muhimu cha ustawi wa uchumi nchini ambapo sekta ya maziwa inachangia lita Billioni 5.3 kila mwaka.
Rais alidokeza kuwa juhudi zilizowekwa zimeimairisha ufugaji kwa asilimia 45 katika kipindi cha miaka mitatu.
Aidha ruto alisema kiwango hicho bado kiko chini ikilinnganishwa na uwezo ambao wafugaji wako nao wa kuzalisha maziwa zaidi.
Wakati uo huo Rais aliwarai waekezaji wa nje kuekeza katika sekta hiyo humu nchini ili kuongeza uzalishaji.
Alisema kupitia uwekezaji wafugaji watawezeshwa zaidi na uchumi wa taifa utaimarika .
“Ufugaji ni sekta muhimu sana kwa ukuaji wa uchumi na endapo itawekezwa itafanya vizuri hivyo serikali inampango wa kutumia tekinolojia kuimarisha ufugaji kwa minajili na kuinua uchmi.
“Kwa hivyo inawaomba muendelee kuekeza zaidi katika sekta hii ili kuongeza uzalishaji.”
Taarifa ya Pauline Mwango
