Wafanyibiashara wa kuuza matunda kaunti ya Kilifi wanalalamikia kudorora kwa biashara

Wafanyibiashara wa kuuza matunda kaunti ya Kilifi wanalalamikia kudorora kwa biashara

Wafanyibiashara wa kuuza matunda kaunti ya kilifi wanalalamikia kudorora kwa biashara zao kufuatia kupungua kwa matunda.

Wakizungumza na Coco Fm wafanyibiashara hao walisema kwa sasa matunda kama vile machungwa, maembe na mananasi yamepotea hali inayofanya biashara zao kudorora.

Kulingana na wafanyibiashara hao gharama ya uzalishaji imekuwa juu na kufanya wakulima wengi kushindwa kuendeleza shughuli za kilimo.

Aidha waliongeza kuwa kwa sasa wanategemea matunda kutoka nchi jirani ya Tanzania hali ambayo inafanya uchumi wa taifa unashuka.

Waliongeza kuwa taifa linaweza kuzalisha matunda kwa kiwango kikubwa na kuimarisha maisha ya wakulima.

Aidha waliitaka serikali kuwawezesha wakulima na mbinu za kisasa hasa  wakulima kutoka maeneo kame pamoja na kupunguza gharama ya uzalishaji ili kuzidisha mapato zaidi.

“ Nchi iko na uwezo mkubwa ya kuzalisha matunda iwapo serikali itawawezesha wakulima kama vile kuwachimbia mabwawa na hata kuwapa mbolea na mbegu”

Taarifa ya Pauline Mwango