Makubaliano ya UDA na ODM

Makubaliano ya UDA na ODM

Mkutano wa wabunge wa bunge la kitaifa na Seneti wa Chama ODM na UDA kuhusu utekelezaji wa mchakato wa ajenda 10 zilizoidhinishwa kati ya Rais William Ruto na Hayati Raila Odinga mwezi Machi mwaka 2025, umefanyika.

Hatua hii inayonyesha utofati wa misimamo ya kisiasa kati ya viongozi wa ODM huku Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, Gavana wa Siaya James Orengo, Mbuge wa Embakasi mashariki Babu Owino wanaopinga ushirikiano ODM na UDA, wakikwepa mkutano huo.

Mwenyeti wa Kamati ya utekelezaji wa mchakato wa ajenda 10, Dkt Agnes Zani wakati wa mkutano huo uliyoandaliwa katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi, alielezea mafanikio ya ajenda 10, akisema mchakato huo hauna mipaka na utaendelea kutekelezwa hadi matakwa ya wakenya yaafikiwe.

Gavana wa Kisumu Prof Anyang’ Nyong’ aliye mwanachama wa ODM, alisisitiza haja ya suala la ugatuzi kutekelezwa kikamilifu sawa na mgao wa serikali hizo kusambazwakwa wakati huku Kiongozi wa wachache bungeni Junet Mohamed akimkumbusha rais Ruto kuhusu deni la shilingi bilioni 12 ambalo chama cha ODM kinadai serikali.

Kinara wa Chama cha ODM Dkt Oburu Oginga alisisitiza kwamba mpango wa serikali jumuishi utaendelea hadi mwaka 2027 pamoja na mchakato wa ajenda 10 kutekelezwa, huku akiitaka serikali kuweka kitengo cha kukabiliana na majanga.

Hata hiyo Rais William Ruto alisema uwajibikaji ni lazima kwa kila kiongozi na mchakato wa ajenda 10 utatekelezwa zaidi huku akihimiza viongozi kujitolea kupambana na ufisadi, akisisitiza huduma zote za kiserikali kupitia mfumo wa kidigitali.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi