Mahakama ya Kilifi imehairisha kesi ya mshukiwa wa wizi wa kimabavu Joel Kalume Diga hadi tarehe 30 mwezi Machi mwaka huu ambapo kesi hiyo itasikizwa.
Hakimu wa Mahakama hiyo James Mwaniki ameagiza mshukiwa Diga kurudishwa rumande hadi wakati wa kusikizwa kwa kesi hiyo.
Wakati wa kikao hicho, Mahakama ilielezwa kwamba Diga alifanya wizi wa kimabavu mwaka 2025 kwa kuiba pikipiki hatua iliyosababisha kuzuka kwa vurugu mjini Kilifi na kutafutwa na umma ambao walikuwa na hamaki yakutaka kumuua.
Mnamo tarehe 17 mwezi Novemba mwaka uliopita, Diga alifikishwa Mahakama baada ya kuponea kifo na kusomewa mashtaka ambapo alikana mashtaka dhidi yake na Mahakama ikamnyima dhamana na kuagiza kuzuiliwa rumande.
Hii ni baada ya ripoti kutoka Ofisi ya jamii katika kaunti ya Kilifi kueleza Mahakama kwamba mshukiwa ni mwizi sugu na umma ina hamaki ya kumuua.
Kesi hiyo itasikizwa tarehe 30 mwezi huu ambapo washahidi watatoa ushahidi wao mbele ya Mahakama hiyo.
Taarifa ya Teclar Yeri
